
Wawakilishi wataka ukarabati wa shule kongwe
Unguja. Licha ya mafanikio ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kujenga shule mpya za kisasa, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema kuna haja ya kuzifanyia ukarabati mkubwa za zamani ili kuleta usawa kwa wanafunzi. Pia wameitaka wizara kutoa ufafanuzi kuhusu miongozo wanayotumia kuita majina shule zinazojengwa, kwani huenda majina ya asili yakapotea…