
Wizara ya Kazi, Uwekezaji kuzalisha ajira 18,500 Zanzibar
Unguja. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji imeainisha vipaumbele vyake ikiwemo kuratibu upatikanaji wa ajira za staha 3,500 nje ya nchi na ajira rasmi 15,000 za ndani. Pia, itaimarisha usalama na afya kazini kwa ununuzi wa vifaa vya uchunguzi, kufanya ukaguzi kazi katika maeneo 600 ya kazi (Unguja 500 na Pemba 100)…