
Mbunge ataka maboresho ya matunzo kwa watoto, ajibiwa
Dodoma. Mbunge wa viti maalumu (CCM), Esther Malleko ameihoji Serikali ni lini itafanya maboresho ya Sheria ya Ndoa ili ikidhi matunzo kwa watoto kwa sababu gharama za maisha zimepanda. Akiuliza swali leo Jumatano, Mei 22, 2024, Malleko amehoji: “Nini kauli ya Serikali kwa wale wanaoshindwa kutekeleza majukumu waliyokubaliana katika vikao vya usuluhishi na kusababisha watoto…