Ripoti yabaini mtumishi Hospitali ya Mnazi Mmoja alishambuliwa

Unguja. Ripoti ya kifo cha mfanyakazi wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja, Said Ali Shineni imebainisha hakikuwa cha kawaida bali alishambuliwa.

Said anadaiwa kuuawa Juni 4, 2024 na walinzi wa hospitali hiyo ambao ni kutoka Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Ripoti ya uchunguzi wa kifo chake iliyotolewa kwa ndugu wa marehemu leo Juni 6, 2024 na ofisa upelelezi wa hospitali hiyo, Juma Vuai imesema kifo hicho kinaonekana hakikuwa cha kawaida, bali kimetokana na shambulizi la waya. Mwili umekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya maziko.

Ndugu hao wametakiwa kuandika barua kwenda Wizara ya Afya ili wapewe ripoti kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine za kisheria.

Akizungumzia suala hilo, Saleh Abdallah Saleh ambaye ni ndugu wa marehemu amesema wamechukua mwili na wanafanya taratibu za maziko leo saa 10.00 jioni katika makaburi ya Mwanakwerekwe.

“Sisi tukiitaka ripoti lazima tuandike barua Wizara ya Afya kupitia mkurugenzi ili tukabidhiwe kwa ajili ya kesi,” amesema.

Amesema mchakato wa kuandika barua utaanza baada ya kukamilisha maziko ya ndugu yao.

Juzi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Mchomvu alisema wanaendelea kufuatilia tukio hilo kupata ukweli.

Alipotafutwa leo Juni 6, msaidizi wake alisema yupo kwenye kikao