NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wazalishaji wa bidhaa za Chuma aina ya Flat Bars, Square and Round Pipes kuzalisha na kuuza bidhaa zilizokidhi viwango ili kuepuka madhara ya kiafya na kiuchumi.

Amesema hivi karibuni wataanza kupita katika viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo kukagua kama wanaendelea kuzalisha bidhaa zisizokidhi viwango na kuweza kuwachukulia hatua ikiwemo kuvifungia viwanda ambavyo havifuate taratibu.

“Taarifa hizo ni muhimu kwa wanunuzi na watumiaji wa bidhaa kwani huwezesha kutoa mrejesho kwa mzalishaji husika pamoja na kufanya ufuatiliaji (tracebility) endapo itabainika kuwa na kasoro yoyote”. Amesema Dkt. Ngenya.

Ameeleza kuwa pamoja na jitihada zilizofanywa na TBS ili kuhakikisha bidhaa hizo zinaandikwa taarifa muhimu ikiwa ni pamoja kutoa muda maalum (grace period) ili kuhakikisha mnatekeleza takwa hilo muhimu, bado kuna baadhi ya wazalishaji ambao hawajatekeleza, na hivyo kusababisha changamoto katika udhibiti.
Hata hivyo amesema TBS haitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria kwa yeyote yule atakayezalisha bidhaa za flat bars, square pipes na round pipes kinyume na matakwa ya viwango.
Kwa upande wake Ibrahimu Haji Kutoka Kampuni ya Alaf, amesema wataendelea kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango ili kuendana na ushindani wa biashara nchini.
Amesema kupitia kikao hicho, watayachukua maelekezo yote ambayo wamepewa na wataalamu kutoka TBS na kuyafanyia kazi ili kuendelea kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango.