Mmoja auawa kwa kupigwa risasi maandamano Kenya

Nairobi. Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Rex Kanyike amefariki dunia kwenye maandamano yanayofanywa na vijana wa Kenya kupinga mapendekezo ya nyongeza ya kodi, Jeshi la Polisi nchini humo limesema leo,  huku waandamanaji wakiitisha maandamano ya kitaifa wiki ijayo. Jeshi la polisi limesema linachunguza madai kwamba mwanaume huyo alipigwa risasi na polisi baada ya maandamano ya…

Read More

Mbinu ya kuharakisha matumizi nishati safi yatajwa

Dar es Salaam. Katika kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) limependekeza ushirikishwaji wa viongozi wa dini na wale wa kimila katika kutoa elimu kwa wananchi. Pendekezo hilo limetolewa leo Juni 21, 2024 na Ofisa Mwekezaji Mwandamizi wa UNCDF, Emmanuel Muro, katika kongamano…

Read More

Vijiji 25 kunufaika biashara ya kaboni Arusha

Arusha. Wananchi katika vijiji 16 vilivyopo Wilaya ya Longido na Monduli (9) mkoani Arusha wanatarajiwa kupata Sh33 bilioni kila mwaka kupitia utekelezaji wa mradi wa uvunaji kaboni. Mradi huo unahusisha kudumisha hatua za uhifadhi wa hekta milioni 2.4 utazalisha tani milioni 1.9 za hewa ya Kaboni zenye thamani ya Dola za Marekani 12.7 milioni, sawa…

Read More

Wananchi kupewa mabomu baridi kukabiliana na tembo Lindi, Ruvuma

Tunduru. Wizara ya Maliasili na Utalii imepeleka askari wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) kuwafundisha wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka hifadhi na mapori, namna ya kukabiliana na wanyamapori, hasa tembo wanaokatisha kwenye makazi yao. Mafunzo haya yanatolewa katika Wilaya za Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma na Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, yakiwa yanahusisha…

Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC

Waziri Kassim Majaliwa Leo Juni 21, 2024 amekutana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Katibu wa Kamati ya CPC Jimbo la Shanxi nchini China. Katika mazungumzo yao ambayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Waziri Mkuu, Magogoni Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu…

Read More

Wahamiaji saba kortini, mmiliki wa ‘shangingi’ bado hajatajwa

Moshi/Dar. Raia saba wa Ethiopia, waliokamatwa Njiapanda wilayani Moshi wakisafirishwa kwa gari aina ya Toyota Land Cruiser namba T888 BTY linalodaiwa kumilikiwa na mbunge, wamefikishwa kortini wakikabiliwa na mashitaka mawili. Ingawa hati ya mashitaka haikutaja nani ni mmiliki wa gari hilo, vyanzo kutoka Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vinaeleza nyaraka za…

Read More

MAJALIWA: TUTAYAENZI MEMA YOTE YALIYOFANYWA NA NZUNDA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wataendelea kumkumbuka na kuyaenzi mema yote yaliyoyafanywa na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 21, 2024) alipokwenda kuhani msiba wa marehemu Nzunda, nyumbani kwa marehemu Goba, Dar es Salaam. Marehemu Nzunda alifariki Juni 18, mwaka huu…

Read More