Dar es Salaam. Baada ya vipeperushi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa mgomo wa wafanyabiashara Soko la Kariakoo, Mwananchi Digital imefika katika soko hilo na mpaka saa 3 asubuhi maduka mengi bado hayajafunguliwa.
Leo Jumatatu, Juni 24, 2024 Mwananchi imeshuhusdia wafanyabiashara katika eneo hilo wakiwa wamekaa nje, huku maduka yao yakiwa yamefungwa.
Baadhi ya machinga katika Soko la Kariakoo wakiendelea na biashara zao leo Jumatatu, Juni 24, 2024. Picha na Aurea Simtowe
Biashara pekee inayoendelea ni ile inayofanywa na wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ katika mitaa mbalimbali sokoni hapo.
Wakati vipeperushi vikisambaa kwenye mitandao ya kijamii vikieleza kuhusu mgomo wa wafanyabiasha Kariakoo kuanzia leo Jumatatu, uongozi wao uliwataka kuwa watulivu, ukisema tamko litatolewa.

Baadhi ya maduka katika Mtaa wa Agrey yakiwa yamefungwa huku wamiliki wake wakiwa nje leo Jumatatu, Juni 24, 2024. Picha na Devotha Kihwelo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Karikaoo, Martin Mbwana akizungumza na Mwananchi Juni 22, 2024 alikiri kuona vipeperushi hivyo, akieleza hiyo ni hasira za kuchoshwa na wanayofanyiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Baadhi ya wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo wakiwa wamekaa nje ya maduka yao leo Jumatatu, Juni 24, 2024. Picha na Aurea Simtowe
Hata hivyo, amewataka watulie akisema wapo jijini Dodoma kushughulikia suala hilo na kwamba, wamepanga kukutana na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba Jumatatu Juni 24.
Endelea kufuatilia mitandao yetu