
Wakulima wa pamba walalamikia mizani kuchakachuliwa
Mwanza. Wakulima wa zao la Pamba mkoani hapa wamelalamikia baadhi ya wanunuzi kuchakachua mizani inayotumika kununulia zao hilo, hali inayowasababishia kupata hasara. Wakizungumza leo Jumatano Juni 26, 2024 na Mwananchi, wakulima hao wamesema kitendo hicho kinawafanya baadhi yao kukata tamaa na kushindwa kuendelea na kilimo hicho. “Mizani inayokuja kupima pamba tunaomba wapimaji wasiwe wanaichezea na…