BINGWA wa mashindano ya CRDB Taifa Cup kwa upande wa wanaume na wanawake atazawadiwa kila moja Sh million 7.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Kanda ya Kati wa beki hiyo, Chabu Mishwaro mjini Dodoma wakati mashindano hayo yakishika kasi kwenye viwanja vya Chinangali, kwa upande wa wanaume na wanawake.
Mishwaro alisema, washindi wa pili kwa pande zote mbili watazawadiwa Sh4 milioni wakati na kufanya jumla ya Sh 22 milioni kutengwa kwa ajili ya zawadi kwa washindi katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na CRDB na Azam Media.
Kwa mujibu wa Mishwaro, kutakuwa na zawadi ya mchezaji mwenye thamani kubwa (MVP) kwa wanawake na wanaume ambao kila mmoja atazawadiwa Sh500,000 ambapo wafungaji bora watazawadiwa Sh 600,000 na Mabeki Bora sh600,000 kila mmoja.
Alisema kutakuwa na zawadi ya Rookien of the year kwa wanaume na wanawake ambapo kila mmoja atapata sh 200,000 na kauli mbiu wanayoitumia katika mashindano hayo ni “Ni zaidi ya Game, ni Maisha”.
“Tumeyapa thamani kubwa mashindano haya kwa kuweza zawadi nono huku tukiingia gharama ya Sh 100 millioni kwa ajili ya vifaa, huku gharama ya za uendeshaji kwa Shiirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania zikiwa Sh milioni 35 na gharama za maandalizi Sh milioni 30 na gharama nyingine za mdhamini ni Sh10.4 milioni. Jumla ya udhamini wote ni sh milioni 200,” alisema Mishwaro.
Alifafanua, lengo kubwa ni kuhakikisha mchezo huu unaendelezwa kwa ukubwa wake ndani na nje ya Tanzania na kuwa mchezo pendwa na wenye manufaaa kwa vijana na Taifa kwa ujumla.
“Kwa kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii “Corporate Social Investment Policy” Benki imeendelea kufanikisha mashindano haya. Mbali ya kuendeleza mchezo, tumetilia mkazo elimu kwa vijana, sera ambayo imeanza tangu mwaka 2020 tulipozindua kwa mara ya kwanza,” alisema.
Alisema pamoja na kutoa fursa kwa vijana ya kuonyesha vipaji vyao na kuboresha afya zao, kupitia mashindano, pia imekuwa ikiwapa ufadhili wa masomo katika vyuo mbalimbali hapa nchini ili kujiendeleza na elimu, kupatiwa elimu ya fedha, ujasiriamali kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa.