
June 30, 2024


PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 1,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 1,2024 Featured • Magazeti About the author

Manji afariki dunia, Yanga wamlilia
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji amefarikia dunia leo Jumapili jijini Florida nchini Marekani baada ya kuugua kwa muda mfupi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Uongozi wa Young Africans Sports Club umethibitisha kifo cha Manji ambaye alikuwa mfadhili wa timu hiyo kuanzia 2012 hadi 2017 Mei alipojiuzulu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu ya Yanga imesema imepokea…

Kigoma na Mara waibuka kidedea msimu wa 4 wa CRDB Bank Taifa Cup
Msimu wa 4 wa mashindano ya mpira wa Kikapu ya CRDB Bank Taifa Cup umehitimishwa siku ya Jumamosi jijini Dodoma katika viwanja vya Chinangali na ambapo mikoa ya Kigoma na Mara imeibuka kidedea kwa upande wa wanaume na wanawake. Mgeni Rasmi katika fainali hizo alikua ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ambae…

10 wateuliwa kuwania uenyekiti CCM, UVCCM
Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewateua makada wake 10 kuwania nafasi za uenyekiti wa mikoa na wilaya mbalimbali. Nafasi hizo ni zile zilizoachwa wazi baada ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Nafasi zilizokuwa wazi ni ya uenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa…

Aweso aagiza vigogo wawili Dawasa wasimamishwe
Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kuwasimamisha vigogo wawili wa mamlaka hiyo, akiwamo Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Kiula Kingu kupisha uchunguzi dhidi yao. Mbali na Kingu, mwingine ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji wa Dawasa, Shaban Mkwanywe. Waziri…

Majaliwa atoa maagizo udhibiti dawa za kulevya, aonya matumizi ya ‘cha Arusha’
Mwanza. Wakati matumizi ya dawa za kulevya yakiathiri vijana zaidi ya 14,874 nchini, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza uandaliwe mpango wa uwezeshaji wa waraibu wa dawa za kulevya waliohitimu matibabu ili kuingia kwenye shughuli za ujasiriamali. Majaliwa ametoa maagizo hayo kwa Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Ofisi ya…

Mambo ya kuzingatia kuepuka saratani ya uume
Dar es Salaam. Saratani ya uume, ugonjwa ambao haujulikani sana kwa wengi nchini Tanzania, unaathiri maisha ya wanaume kwa kiwango kikubwa. Wakati mwingine, matibabu pekee yanayopatikana ni kukatwa uume, hali inayobadilisha kabisa maisha ya mgonjwa. Ingawa ni nadra na mara nyingi haijadiliwi wazi, saratani hii inachukua asilimia 27 ya saratani zote kwa wanaume nchini na…

Msigwa arusha kombora Chadema, wamjibu lilikuwa ni suala la muda tu
Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa amesema uamuzi wake wa kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) umechochewa na hatua ya Chadema kukosa misingi na uhalali wa kukikosoa chama hicho tawala. Katika mazingira hayo, amesema hakuona haja ya kuendelea kushindana, badala yake aungane na Serikali katika mambo inayoyafanya ikiwamo amani, utulivu…

Wadau wataja mambo manne kufanikisha upatikanaji katiba mpya
Mwanza. Wadau mbalimbali jiji hapa wamependekeza suala la upatikanaji wa Katiba mpya lirejeshwe bungeni likajadiliwe upya ili kuruhusu mchakato uendelee. Mapendekezo mengine ni kuitishwa kwa mkutano maalumu wa kitaifa wa kujadili Katiba mpya, kuunda timu ya wataalamu wa kuchukua maoni na mapendekezo yatakayotolewa katika mkutano huo, lakini pia kuandika rasimu mpya itakayotokana na maoni na…