
Serikali ilivyojipanga uboreshaji milki za ardhi
Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesaini mkataba wa Sh346 bilioni na Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi. Mradi huo unalenga kuimarisha usalama wa milki za ardhi na kuwezesha miundombinu ya usimamizi wa rasilimali hiyo nchini. Majaliwa amesema hayo leo Juni 28, 2024…