Zaidi ya Milioni 1 wamelazimika kuhama Rafah – UNRWA
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema kuwa wakimbizi wa kulazimishwa kuhama makazi yao wamefikia zaidi ya watu milioni moja kutoka mji wa Rafah kusini mwa Gaza. Jeshi la Israel limewaambia raia kwenda kwenye “eneo lililopanuliwa la kibinadamu” lililo umbali wa kilomita 20 (maili 12). Wapalestina wengi wamelalamika kuwa wako…