
Zuma atoa onyo iwapo IEC itatangaza matokeo ya uchaguzi leo
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ametishia kuchukua hatua ya kisheria ya kuizuia Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo (IEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu leo Jumapili kama ilivyoratibiwa. Zuma alitoa onyo hilo jana, baada ya chama chake cha Mkhonto weSizwe (MK) kutaka uchaguzi huo ufanyike upya, kikidai kuwa tayari kimewasilisha ithibati na vielelezo…