
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 2,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 2,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 2,2024 Featured • Magazeti About the author
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam June 2, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania. The post Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 2, 2024 first appeared on Millard Ayo.
Raisa Said,Tanga WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri zote nchini, kuhakikisha kwenye maeneo yao zinaanzisha madawati ya sayansi,teknolojia na ubunifu, ili kuweza kukuza na kulea bunifu mbalimbali katika halmushauri kwa vijana waliopo kwenye sehemu hizo. Hayo aliyasema.wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kitaifa ya elimu,ujuzi na ubunifu 2024 ,yaliofanyika mkoani Tanga. Alisema kwa kufanya hivyo…
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof….
Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital Wazazi wa wanafunzi wa shule ya chekechea ya Busy Bees wamefurahishwa na vipaji vilivyooneshwa na watoto wao wakati waliposhindana katika michezo mbalimbali ikiwamo soka. Wanafunzi hao wameshiriki michezo hiyo leo Juni Mosi, 2024 Upanga, jijini Dar es Salaam katika siku maalumu ya michezo ‘Annual Sports Day’ inayoandaliwa na uongozi wa…
Babati. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimechukua na kinakwenda kufanyia kazi mapendekezo ya wanachama wake mkoani Manyara wanaotaka wagombea udiwani na ubunge kuchaguliwa na wanachama na si wajumbe. Ushauri huo wameutoa leo Jumamosi, Juni 1, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya zamani ya Babati Mjini, uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk…
Na Mwandishi wetu, Michuzi Tv GS1 Tanzania wazindua Barcodes Charity Wark kwa lengo la Kusaidia wanawake 100 kutoka kila Wilaya hadi kufikia Wanawake 18300 ili kupata alama ya msimbomilia (Barcodes) katika bidhaa wanazozizalisha. Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo, Juni Mosi, 2024, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Viwanda…
Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameanza ziara ya wiki tatu Mkoa wa Singida ambako atafanya mikutano ya hadhara katika kata zote kwenye kila wilaya. Lissu ambaye ameongozana na viongozi kadhaa wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema (Bazecha), Hashim Juma wameanza na Jimbo la Iramba Magharibi linaloongozwa…
Mtafiti wa Udongo na Mbolea wa Kituo cha Serian Arusha Richard Temba akionesha Utafiti wa Mbolea unaotokana na taka ambazo baada ya uhifadhi zinazalisha minyoo ya kufanya uchakataji wa Mbolea ambapo Elimu ya Utafiti na Ubunifu ulitolewa katika Maadhimisho ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga….
Geita. Watanzania wametakiwa kuacha kuendelea kuona mabadiliko ya tabia nchi kama changamoto badala yake waitumie kama fursa ya kiuchumi kwa kupanda miti na kuitunza ili kufanya biashara ya hewa ukaa inayohimizwa na jumuiya ya kimataifa. Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira, Cyprian Luhemeja ameyasema hayo wakati wa shughuli ya upandaji…