ANC isipofikisha asilimia 50 ya kura, hiki kitatokea

Johannesburg. Ni wazi kwamba Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini kimeporomoka kimvuto na ushawishi kwa wapigaa kura.  Kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo ilipopata uhuru miaka 30 iliyopita ANC imepata asilimia 40 ya kura, hivyo kitalazimika kuungana na chama kingine kuunda serikali. Kutokana na anguko hilo, sasa viongozi wa ANC wanajipanga…

Read More

Simba SC yaingilia dili la winga Yanga

MABOSI wa Simba wajanja sana. Kwa sasa wameamua kufanya mambo yao kimyakimya katika kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao ili kurudisha heshima mjini na hivi unavyosoma Mwanaspoti wanafanya mazungumzo na mawinga wawili wa maana wa DR Congo, akiwamo anayewaniwa na Yanga. Mwanaspoti limepenyezewa taarifa kwamba, pale DR Congo Simba imefanya mazungumzo na winga …

Read More

Jamii yahimizwa kulinda, kuheshimu haki za watoto

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Wakati dunia ikisherehekea Siku ya Kimataifa ya Watoto, wito umetolewa kwa jamii kuheshimu haki za watoto na kuhakikisha wanalindwa wakati wote. Siku ya Kimataifa ya Watoto huadhimishwa Juni Mosi kila mwaka kwa lengo la kutambua umuhimu wa watoto katika jamii na kuangazia haki na ustawi wao. Naibu Mkurugenzi wa Kampuni…

Read More

Usajili matibabu bure kwa makundi maalumu mbioni

Unguja. Wasimamizi wa jumuiya zinazohudumia kaya masikini na watoto yatima,  wametakiwa kusimamia kikamilifu usajili wa kundi hilo katika Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) ili kuwarahisishia kupata matibabu.  Pia, wadau wa maendeleo na watu wenye uwezo,  wameombwa kujitokeza kuchangia mfuko huo kulisaidia kundi hilo. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZHSF, Yaasin Ameir Juma ametoa kauli…

Read More

TBS YASISITIZA WAFANYABIASHARA KUZINGATIA VIWANGO

Raisa Said, Tanga Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) limesisitiza wafanyabiashara kuzingatia bidhaa zao zimekidhi matakwa ya viwango kwani kwa wale wasiofuata taratibu hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kupigwa faini kuanzia million 10 hadi million 100. Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Masoko TBS Gladness Kaseka wakati akizungumza na waandishi wa habari na Wadau…

Read More

Mkondo wa maji chini ya ardhi waibua hofu Moshi

Moshi. Maji yanayotoka chini ya ardhi katika makazi ya wananchi na baadhi ya maeneo ya biashara eneo la Ngangamfumuni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, yameibua hofu ya usalama. Kwa mara ya kwanza maji yaliibuka mwaka 2020 na kuathiri shughuli za ujenzi wa mradi wa kimkakati wa mkoa huo wa stendi ya kimataifa ya mabasi ya…

Read More

Jaji Tiganga ataka ushiriki wa sekta binafsi udhibiti taka ngumu

Arusha. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Joachimu Tiganga ameitaka Serikali kuishirikisha sekta binafsi na kuweka mazingira wezeshi ya kusaidia katika udhibiti wa taka ngumu zinazozagaa mitaani. Jaji Tiganga amesema kuwa zaidi ya tani milioni saba za taka ngumu zinazozalishwa nchini, ni asilimia 35 pekee ndizo zinazokusanywa na kuteketezwa, huku zingine…

Read More

Chadema Morogoro mjini wapata viongozi wapya

Morogoro. Baada ya vuta nikuvute ya uchaguzi viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Morogoro mjini, hatimaye chama hicho kimepata viongozi wapya wa jimbo na mabaraza watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo leo Juni Mosi, 2024, msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu na operesheni kamanda…

Read More