
Profesa Janabi awamulika walaji wa nyama choma Arusha
Arusha. Matumizi ya chumvi yaliyopitiliza yametajwa kuwa chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wengi wa Mkoa wa Arusha, ikiwemo kiharusi, shinikizo la juu la damu, figo, na magonjwa ya moyo. Mkoa huo umetakiwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti kiwango kikubwa cha shinikizo la juu la damu linalowakabili wananchi wengi. Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Juni 27,…