
Walioshtakiwa wakidaiwa kumuua Mawazo waachiwa huru
Geita. Mahakama Kuu Kanda ya Geita imewaachia huru washtakiwa wanne waliokuwa wakikabiliwa na shtaka la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo. Hukumu hiyo imetolewa juzi Juni 25, 2024 na Jaji wa Mahakama hiyo, Graffin Mwakapeje baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo. Washtakiwa…