Mbowe, Semu wachaguliwa kuiongoza TCD
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Sambamba na Mbowe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kituo hicho. Mbowe anashika nafasi hiyo akimrithi, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba…