Rais Ruto aapa kutokomeza maandamano ya vurugu – DW – 26.06.2024
Ruto ameapa kwamba matukio ya uvamizi wa Bunge aliyoyaita “kitisho kwa usalama wa taifa”, kamwe hayatojirudia kwa gharama yoyote.” Hayo yanajiri wakati jumuiya ya kimataifa ikielezea wasiwasi wake kutokana na hali ya vurugu inayoshuhudiwa nchini humo. Kupitia televisheni, Rais William Ruto wa Kenya ameapa kuchukua msimamo mkali dhidi ya “vurugu na machafuko” yaliyoshuhudiwa hapo jana…