PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 26,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 26,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUNI 26,2024 Featured • Magazeti About the author
Dar es Salaam. Wanafunzi 100 kutoka shule za sekondari nchini, wameanza kunolewa kupitia programu ya uongozi kwa vijana (Beginit), iliyotajwa kuwa chachu ya mabadiliko katika uongozi wa kijamii hapo mbeleni. Wadau wa maendeleo wanaoendesha mradi huo, wamebainisha kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali kutoa mafunzo ya uongozi kwa vijana lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutambua…
Moshi. Kesi ya mauaji inayomkabili mkazi wa Katanini, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Beatrice Kwai (36) anayetuhumiwa kumuua mumewe, Evagro Msele (43) imepigwa kalenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi hadi Julai 8, 2024. Tukio hilo la mauaji ya mfanyabiashara huyo maarufu mjini hapa, lilitokea usiku wa Mei, 25 2024 katika Kitongoji cha Pumuani A,…
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Kasilda Mgeni amewaonya baadhi ya wazazi wanaotumia kesi za ukatili wa kijinsia kwa watoto kama mtaji kulipana fedha pindi anapofanyiwa ukatili kuacha mara moja tabia hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuathiri saikolojia na afya ya mtoto pamoja na kumfanya ashindwe kutimiza ndoto zake. Ameeleza hayo kwenye mkutano…
Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka watathmini mazingira na wawekezaji kulipa Ada za Tathmini ya Mazingira (EIA) katika wakati uliopangwa ili kutekeleza miradi yao kwa kuzingatia sheria za mazingira. NEMC imesema muda unaotakiwa kulipwa ada na tozo hiyo kisheria ni kuanzia Julai mosi hadi Desemba 31 kila…
* picha za mabondia kuwekwa katika kuta za ubalozi wa Ufaransa nchini na Houlgate, Normandy na Paris nchini Ufaransa Na Leandra Gabriel, Dar es Salaam SERIKALI Ya Ufaransa kupitia Ubalozi wake nchini imeeleza kuwa suala la ushiriki wanawake katika michezo na kuendeleza vipaji ni moja ya kipaumbele chao na hiyo ni pamoja na kuhakikisha wanawake…
Dar es Salaam. Tanzania imeweka lengo la kuvutia mitaji ya Sh261 bilioni kila mwaka kutoka kwa wawekezaji nchini Uturuki kupitia sekta kadhaa za uwekezaji, ikiwamo kilimo. Ili kufikia malengo hayo, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeingia mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Africapital Investiment Holding Limited ambayo itafanya kazi ya kuvutia mitaji na…
Mwandishi Wetu, Dodoma. WASHINDI wa Kampeni ya Weka, Tumia na Ushinde Kutoka Benki ya NMB, jana walikabidhiwa zawadi huku umati mkubwa wa wakazi wa Dodoma ukishuhudia tukio hilo. Kutolewa kwa zawadi hizo ni hitimisho la Kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyofikia mwisho wake Mei mwaka huu ambapo zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh250…
Dar es Salaam. Wizara ya Maliasili na Utalii imesema idadi ya faru imeongezeka kutoka 161 mwaka 2019 hadi kufikia 253 mwaka jana kutokana na matumizi ya teknolojia ya ulinzi waliyowekewa iitwayo Transmitters. Hayo yamebainishwa hii leo Jumanne ya Juni 25, 2024 katika warsha iliyoandaliwa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), iliyowakutanisha wataalamu wa…
-Kituo cha kupoza umeme kujengwa Nkansi-Maeneo 1,500 yaliyofanyiwa mapitio yamekidhi vigezo kulipia 27,000/- Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema changamoto ya umeme katika Mkoa wa Rukwa itamalizika baada ya Mkoa huo kuunganishwa katika Gridi ya Taifa kupitia Mradi wa njia ya kusafirisha Umeme wa Msongo wa Mkubwa wa Kilovolti 400 wa Tanzania –…