Wananchi Zanzibar kununua umeme popote kidijitali

Unguja. Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) limeingia makubaliano na taasisi sita kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo popote kidijitali, kwa lengo la kuleta ufanisi na kuwaondolea wateja usumbufu. Akizungumza kwenye hafla ya kufikia makubaliano hayo leo Jumapili, Juni 30, 2024, Meneja wa shirika hilo, Haji Mohammed Haji amesema mbali na kuwaondolea wananchi usumbufu na…

Read More

Kigoma, Mara zabeba ndoo Taifa Cup

TIMU ya kikapu ya wanaume ya Kigoma na wanawake ya Mara zimeibuka mabingwa wa mashindano ya Kikapu ya Taifa (CRDB Taifa Cup) yaliyomalizika juzi Jumamosi usiku kwenye Uwanja wa Chinangali, jijini Dodoma. Kigoma ilishinda taji hilo kwa kuifunga Dodoma kwa pointi 58-54, ilihali Mara ilipata ushindani mkali kuifunga Unguja kwa pointi 57-56 katika mchezo wa…

Read More

Sarah awasha moto Msoga Marathoni

WAKATI Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete akiwaita wanariadha kujifua mjini Msoga na kuahidi kuwapa sapoti, mwanariadha maarufu nchini, Sarah Ramadhan ameibuka mshindi wa mbio za Msoga Marathoni zilizofanyika wikiendi iliyopita, huku akifuatiwa na mkali mwingine Failuna Abdi. Tuanze na JK. Rais Kikwete aliyeongoza mbio ya Msoga Half Marathoni iliyofanyika kwa mara…

Read More

Alliance, Harab Motors tishio Ligi ya Caravans

LIGI ya Kriketi ya Caravans T20 ilikuwa njema kwa timu za Alliance Caravans na Harab Motors baada ya timu hizo kupata matokeo mazuri katika michezo iliyochezwa kwenye viwanja vya Dar Gymkhana na Anadil Burhan jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. Mechi ya kusisimua sana ya mwishoni mwa juma iliwakutanisha Alliance Caravans na Generics Gymkhana…

Read More

Simba yasajili viungo wa Yanga

HATIMAYE Simba Queens imekamilisha usajili wa viungo wawili wa Yanga raia wa Nigeria, Precious Christopher na Saiki Atinuke kwa mkataba wa mwaka mmoja. Wachezaji hao wawili wamecheza Yanga kwa misimu miwili wakisajiliwa Septemba 2022, Precious ambaye ni kiungo mshambuliaji na Saiki anayemudu kucheza kiungo mkabaji. Viungo hao wako huru kwa sasa baada ya kumaliza mikataba…

Read More

Abuni kifaa cha kuongeza usikivu cha bei nafuu

Dar es Salaam. Huenda watu wenye changamoto ya usikivu wakapata ahueni zaidi, baada ya mwalimu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) kubuni kifaa kinachoweza kuwasaidia kusikia vizuri. Kubuniwa kwa kifaa hicho nchini, kutashusha gharama za ununuzi ambazo watu wenye changamoto hiyo walikuwa wakizipata katika kununua vifaa kutoka Sh 500,000 kwa kifaa cha sikio…

Read More

Rais Nyusi mgeni rasmi ufunguzi maonyesho ya Sabasaba

Dar es Salaam. Ushirikiano katika sekta za habari, afya na elimu ni miongoni mwa mambo watakayojadili Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Felipe Nyusi. Wakuu hao wa nchi, wanatarajiwa kukutana Julai 2, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo maalumu, baada ya Rais Nyusi kuwasili nchini kesho Jumatatu,…

Read More