120 kuliamsha Lugalo Open 2024
Wachezaji zaidi ya 120 wa gofu wanatarajia kushiriki katika mashindano ya wazi ya ‘Vodacom Lugalo Open 2024’. Mashindano hayo, yalioandaliwa na klabu ya Lugalo yatafanyika kwenye viwanja vya klabu hiyo kati ya Julai 5-7. Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo aliliambia Mwanaspoti, klabu zote za hapa nchini zimealikwa pamoja na wachezaji…