
32,000 wahudumiwa kambi ya madaktari bingwa Arusha
Arusha. Jumla ya watu 32,186 wamehudumiwa katika kambi ya madaktari bingwa na wabobezi iliyokamilika leo Jumatatu Julai mosi, 2024 katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Akitoa tathmini ya kambi hiyo iliyofanyika kwa siku nane, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkombachepa, amesema kati ya watu hao, wapo watoto 4,616 waliohudumiwa katika kambi…