Afisa Masoko na
Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji, Bw. Rahim
Mwanga (Kushoto), akitoa elimu kuhusu huduma na fursa zinazopatikana
katika mfuko huo kwa mwananchi alietembelea Banda la Wizara ya Fedha
katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika
katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar
es Salaam.
Afisa Mikopo kutoka Mfuko
wa SELF Microfinance, Bw. Joackim Gama (Kulia), akiwaelezea baadhi ya
wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, fursa ya mikopo
inayotolewa na Mfuko huo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa
(Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya
Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wizara ya
Fedha, wakimsikiliza Mkazi wa Kigamboni, Bw. Balozi Iddi (kulia),
akiuliza maswali mbalimbali kuhusu elimu ya fedha, wakati alipotembelea
Banda la wizara hiyo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa
(Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya
Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu kutoka Idara
ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Boniphace Kirindimo (Kulia),
akimwelezea Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi
Serikalini, Prof. Geraldine Rasheli, namna ambavyo uandaaji wa bajeti
ya Serikali unavyofanyika, wakati alipotembelea Banda la Wizara, katika
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika
viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es
Salaam.
Mratibu
Mkuu wa Udahili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Bw.
John Adelhardus, akimweleza Mwananchi kuhusu fursa ya kozi mbalimbali
zinazotolewa na Chuo hicho, wakati alipotembelea Banda la wizara ya
Fedha, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)
yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa,
Temeke, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)