
Naibu Waziri ang’aka mradi wa maji kusuasua, atoa maagizo manne
Geita. Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew, amesema hajaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji katika miji 28 baada ya kubaini kuwa ni asilimia 18 pekee ya kazi imekamilika. Akizungumza leo Jumamosi Julai 20, 2024, baada ya kutembelea mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Afcons ya India, naibu waziri huyo amesema hadi sasa utekelezaji hauridhishi…