
Anayeuguliwa na mtoto adai kukimbiwa na mume, atolewa vyombo nje kisa kodi
Morogoro. Evelina Sales, mkazi wa Lukobe, Manispaa ya Morogoro, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukimbiwa na mumewe akidai ni kutokana na mtoto wao kuugua muda mrefu. Mbali na kukimbiwa na mume, mama huyo amesema wakati amelazwa na mwanawe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, mwenye nyumba wake alimtolea vyombo nje kwa sababu alikuwa hajamlipa kodi…