
Je, Wajerumani wanauonaje urathi wa Angela Merkel? – DW – 18.07.2024
Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel amestaafu tangu karibu miaka miwili na nusu. Taasisi ya uchunguzi wa maoni ya YouGov ilifanya uchunguzi wakilishi kwa watu 2,300 nchini Ujerumani kutaka kufahamu namna wanavyomkumbuka. Asilimia 61 walisema hali ya nchi imekuwa mbaya tangu Merkel aondoke madarakani. Walipoulizwa kuhusu sababu za hili, asilimia 28 walisema kuwa “uongozi mbovu” ya serikali…