
Yanga kuwafuata Wajerumani Sauzi kesho
KIKOSI cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini kesho Alhamisi kwenda kuweka kambi ya wiki kama mbili katika jiji la Mpumalanga, Afrika Kusini. Kama ambavyo awali Mwanaspoti iliporipoti, Yanga kupitia Msemaji wake Ally Kamwe amethibitisha safari hiyo ambapo kikosi hicho kitaondoka kesho saa 7 mchana. Kamwe amesema, Yanga ikiwa huko itaweka kambi fupi pamoja na kucheza mechi…