
Wazazi ‘wanavyopigwa’ michango ya mitihani wanafunzi kidato cha nne
Joto ni kubwa kwa walimu, wanafunzi na wazazi katika maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne. Katika maandalizi ya mitihani hii, ambayo kitaalamu tunaweza kuibatiza kama ‘tathmini tamati’, wazazi wanaosomesha watoto shule za binafsi huwa katika wakati mgumu, kwani michango mbalimbali kwa wamiliki wa shule huwa haimithiliki. Katika kipindi hiki, ada rasmi hubaki pale pale…