
Siku 3,074 za Kinana CCM kwa mtindo wa kuombwa, kujiuzulu
Aprili Mosi, 2022, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana, alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara. Nilifanikiwa kuzungumza na Kinana muda mfupi baada ya uchaguzi huo na nikamuuliza swali, kwa nini ameamua kugombea tena nafasi hiyo. Alinijibu kwa kifupi: “Nimeombwa kumsaidia mama.” Ni kipindi ambacho Rais Samia Suluhu Hassan, alikuwa akitimiza mwaka mmoja…