
Maghorofa Dar yashuka bei, kiini chatajwa
Matokeo ya sensa ya majengo ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya majengo yote Tanzania ni 14,348,372 ambapo 13,907,951 yapo Tanzania Bara na majengo 440,421 yapo Tanzania Zanzibar. Aidha majengo mengi (asilimia 94.4) Tanzania siyo ya ghorofa. Majengo tisa kati ya kumi ni kwa ajili ya makazi na asilimia 3.4 ni ya biashara – makazi….