
MIRADI IKAMILIKE, IANZE KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI – WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza miradi yote inayojengwa kwa fedha za Serikali ikamilike ndani ya mwaka huu na ianze kutoa huduma kwa wananchi. Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatatu, Julai 8, 2024) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa. Amesema uimara wa Serikali yoyote…