
Michango yamtoa gerezani aliyechoma picha ya Rais
Mbeya. Siku nne tangu kijana Shadrack Chaula (24), aliyechoma picha ya Rais kuhukumiwa kulipa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka miwili, hatimaye michango ya wananchi imefanikiwa kumtoa katika Gereza la Ruanda Mkoa lililoko mkoani Mbeya. Shadrack aliyekamatwa kwa madai ya kuchoma picha ya Rais Samia Suluhu Hassan na kushtakiwa kwa kosa la kutoa…