
Mbowe akerwa na kodi kwa masikini
Mwanga. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza kukerwa na utitiri wa kodi wanazotozwa wananchi bila kuzingatia uhalisia wa vipato vyao, akisema kinachofanyika ni kuwakandamiza zaidi. Kwa mujibu wa Mbowe, kanuni sahihi ya utozaji kodi ni kuhakikisha anayelipa ni yule mwenye kipato cha ziada na sio wananchi wote. Mbowe ameyasema hayo leo, Jumapili Julai 7, 2024…