Makalla aanza ziara Dar, kinachomsubiri hiki hapa

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla leo Jumapili Julai 7, 2024 ameanza ziara ya kukagua uhai wa chama hicho katika wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam, akianzia Ilala ambako huenda akakumbana na kilio cha miundombinu ya barabara. Katika ziara hiyo ya siku sita,…

Read More

Picha| Tikiti la kampuni ya East West Seed

Balozi wa Kampuni ya East West Seed yenye Makao Makuu yako mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Msanii Mrisho Mpoto, akionyesha Tikiti Maji lililozalishwa na kampuni hiyo Dar es Salaam Leo Julai 7,2024 Kiwakati wa Maonyesho ya 48 ya Biashara maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ya Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji. Kulia ni Afisa Kilimo…

Read More

BoT yawatangazia kiama wanaotoza asilimia 10 ya mikopo

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezitaka taasisi ndogo za fedha nchini kutoza riba ya asilimia 3.5 kwa mwezi kwa mikopo na watakaokiuka kuchukuliwa hatua ikiwemo kufutiwa leseni. Maagizo hayo yamekuja baada ya kuwepo kwa matukio mengi ya taasisi hizo kutoza viwango vya hadi asilimia 10 kwa mwezi kwa kila mkopo jambo ambalo…

Read More

BANDA LA TPA SASA LAENDELEA KUWA KIVUTIO KWA WANANCHI

Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) limeendelea kuwa kivutio kwa Wananchi mbalimbali wanaotembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wananchi wengi wanaotembelea Banda hili wamefurahishwa na huduma zinazotolewa hasa elimu ya kuhusu huduma za Kibandari na…

Read More

IGP WAMBURA ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura akiwa katika picha mbalimbali na watoto waliotembelea Banda la Polisi katika Maonesho ya 48 ya Sabasaba. IGP Wambura ametembelea Maonesho ya Sabasaba na pia kutembelea Banda la Jeshi la Polisi ili kuona namna vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya Jeshi hilo vinavyotoa elimu kwa wananchi.

Read More

Giniki, Angelina wafunika Lake Victoria Marathon 2024

WANARIADHA Shing’ade Giniki na Angelina John wameibuka washindi wa mbio za Lake Victoria Marathon 2024 zilizofanyika leo Jumapili Julai 7, 2024 kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa zikishirikisha wanariadha kutoka mikoa mbalimbali nchini. Giniki ambaye msimu uliopita alimaliza wa pili, amekuwa mshindi wa kwanza kwa wavulana Kilometa 21 katika mbio hizo zilizoanza saa 12 asubuhi…

Read More

Kampuni ya SDIG yaahidi kudumisha uhusiano wake na Tanzania kwa manufaa ya wananchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Kampuni ya Shudao Investment Group (SDIG) ya China, yenye historia ya zaidi ya miaka 70, imeahidi kuongeza ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali kwa lengo la kuleta manufaa kwa Watanzania. Ushirikiano huu, uliodumu tangu mwaka 2006, unalenga kuimarisha sekta ya miundombinu nchini Tanzania na Afrika kwa…

Read More