Wasanii wa Tanzania wakutana na star mkubwa sana wa Korean drama, Son Ye-jin.

Balozi wa Tanzania Korea, Mh. Togolani Edriss Mavura ameambatana na wasanii aliowaalika kufanya ziara Korea kusini kwaajili ya kuimarisha mahusiano na kubadilishana ujuzi katika soko la filamu. Wasanii walikutana na Son Ye-jin kubadilishana mawazo na kisha kukaa na watengeneza filamu wakubwa Cheol-ha Lee na Yohwan KIM. Director Cheol-ha Lee amesema yupo katika maandalizi ya filamu…

Read More

Rombo sasa kulima migomba kwa matone

Rombo. Wataalamu zaidi ya 25 kutoka Wizara ya Kilimo wanatarajiwa kupiga kambi katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,  kutoa elimu ya namna bora ya kuzalisha zao la ndizi kwa kutumia umwagiliaji wa matone na kuachana na kilimo cha mazoea,  ili kuzalisha kwa tija na kuuza bidhaa hiyo katika masoko ya kimataifa. Wilaya ya Rombo ni…

Read More

Mtanzania ahukumiwa kunyongwa China, wengine 26 wakamatwa

Dar es Salaam. Mtanzania mmoja amehukumiwa kunyongwa hadi kufa nchini China kutokana na madai ya kujihusisha na dawa za kulevya, huku wengine 26 wakikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo haramu. Kwa mujibu wa taarifa iliyosambaa mitandaoni, Mtanzania huyo ambaye jina lake halijapatikana mara moja, amehukumiwa kunyongwa katika mji wa Guangzhou nchini humo. Taarifa hiyo inaeleza…

Read More

Uhamiaji yapewa nafasi ya Chipukizi CAF

KLABU ya Uhamiaji imepata nafasi ya kuiwakilisha Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao 2024-2025. Hiyo ni baada ya mabingwa wa Kombe la FA Zanzibar, Chipukizi FC kujiondoa katika uwakilishi huo ikidaiwa sababu kubwa ni ukata ilionao. Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Uhamiaji, imebainisha kwamba nafasi hiyo wameipata baada ya ZFF kufuata…

Read More

Wadau mkoani Mara walia na uwekezaji hafifu

Musoma. Wadau wa maendeleo mkoani Mara wamesema kasi ya uwekezaji mkoani humo bado iko chini,  licha ya mkoa huo kuwa na fursa nyingi za kiuchumi na uwekezaji, hivyo wameitaka Serikali kufanya jitihada zaidi zitakazosababisha kuongezeka zaidi na kuboresha uchumi wa mkoa. Wadau hao wamebainisha hayo Julai 5, 2024 kwenye mdahalo kuhusu uwekezaji ulioandaliwa na Klabu…

Read More