
Mwanafunzi darasa la saba ajiteka na mdogo wake, ataka fedha kwa mama
Mwanza. Katika hali isiyo ya kawaida, mwananfunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Isenga wilayani Ilemela (jina limehifadhiwa) anadaiwa kuiba Sh150,000 kisha kujiteka yeye na mdogo wake wakati wanakwenda shuleni. Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Julai 5, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema baada ya mtoto huyo…