
Shahidi amtambua jaji kama mtuhumiwa wa mauaji
Geita. Katika hali isiyotarajiwa, shahidi wa tatu kwenye kesi inayomkabili Zephania Ndalawa anayeshtakiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia, amemtambua Jaji Graffin Mwakapeje kama mtuhumiwa wa mauaji ya Thomas Masumbuko. Shahidi huyo, Salome Cheyo (9) akiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Musa Mlawa alipotakiwa kwenda kumuonyesha mtuhumiwa kama anamkumbuka, alitoka kizimbani na kwenda hadi alipo…