
Labour yatabiriwa kuwagaragaza Conservative uchaguzi UK – DW – 03.07.2024
Raia kote nchini Uingereza watapiga kura zao kuanzia saa moja asubuhi siku ya Alhamisi, huku uchunguzi wa maoni ukibashiri chama cha Labour kitashinda uchaguzi wake mkuu wa kwanza tangu 2005, na kumfanya kiongozi wake Keir Starmer kuwa waziri mkuu mpya. Matokeo hayo yatashuhudia Uingereza ikirudi kwenye mrengo wa wastani wa kushoto baada ya karibu muongo…