
Madiwani wawili wa upinzani Mchinga watimkia CCM
Mchinga. Madiwani wawili kutoka Kata za Milola na Rutamba zilizopo katika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuvutiwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na unaofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Madiwani hao ni Hussen Kimbyoko kutoka Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na Athumani Mmaije kutoka…