
Israel yataka kuubadilisha mpango wa kusitisha vita Gaza – DW – 26.07.2024
Hatua hii inatatiza mchakato wa kufikiwa makubaliano ya mwisho ya kusitisha mapigano yanayoendelea kwa miezi tisa sasa na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye eneo hilo. Duru kutoka magharibi pamoja na Misri zimearifu leo kuhusiana na nia hiyo ya Israel ya kutaka kubadilisha mkondo kwenye mpango huo. Israel inasema Wapalestina waliokimbia makazi yao wanatakiwa kuhakikiwa wakati wanarejea…