
Korosho Cup kuanza kutimua vumbi Agosti Jimbo la Lulindi
Na Mwandishi Wetu LIGI soka ya Korosho Cup Cup inatarajia kuzinduliwa Agosti 10 mwaka huu katika Jimbo la Lulindi, Masasi, mkoani Mtwara huku zawadi nono zikitangazwa kwa washindi. Mwandaaji na Mdhamini wa ligi hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Utalii 255 Community, Angelina Malembeka, amesema, bingwa atazawadiwa pikipiki ya magurudumu matatu maarufu kama guta…