
Mtu 1 mbaroni kwa kufanya biashara ya kubadilisha fedha bila kibali
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Samwel Mbise (42) mkazi wa Sanawari Jijini Arusha akiwa anafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila ya kuwa na kibali. Akitoa taarifa hiyo leo Julai 31, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi…