
UCHAMBUZI WA MALOTO: Kamala Harris anavyompima ubavu Trump
Ilionekana ingekuwa rahisi kwa Hillary Clinton, kumshinda Donald Trump mwaka 2016, haikuwezekana. Sasa, Kamala Harris anakaribia kuvalishwa glovu, ili aingie ulingoni dhidi ya Trump. Swali ni je, ataweza? Rais wa Marekani, Joe Biden, amesalitiwa na umri pamoja na uchovu wa mwili. Ametii sauti ya Democrats wenzake wengi, walioona asingetosha kushindana na Trump. Biden amevua glovu,…