
Mwili wa mwanamke wakutwa ukielea bwawani
Songwe. Mwili wa mwanamke mmoja ambaye hajafahamika, umekutwa ukielea katika Bwawa la Mbimba, linalotumika kwa shughuli za umwagiliaji kando ya Barabara ya Tanzania – Zambia wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe. Mwili huo umekutwa umeharibika na uliopolewa jana Jumanne Julai 30, 2024 jioni na haijulikani mwili huo kama umetupwa au mtu huyo alitumbukia mwenyewe bwawani humo….