
NIKWAMBIE MAMA: Anguko letu ndiyo fursa yao, tusikubali
Nianze kwa kukupa pongezi kwa kuhimiza uhifadhi wa mazingira pamoja na kupanda miti. Usemi wako wa “Turekebishe pale tulipopaharibu” umekuwa na maana kubwa kwa Watanzania na wengi wetu tunaunga mkono jitihada hizi kwa moyo mmoja. Vijana kwa wazee sasa wameamshwa na maendeleo ya matumizi ya nishati salama na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa….