Novatus aondoka Shakhtar ajiunga Goztepe

Kiungo Mtanzania Novatus Dismas Miroshi (21) amejiunga na Club ya Goztepe ya Uturuki kwa Mkataba wa miaka minne baada ya kumaliza Mkataba wake wa Mkopo Shakhtar Donetsk ya Ukraine. Novatus msimu uliopita alicheza Shakhtar aliyojiunga nao akitokea Zulte Waregem ya Ubelgiji kwa Mkopo wenye kipengele cha kununuliwa moja kwa moja lakini hilo halikufanikiwa. Goztepe ni…

Read More

SMZ yatoa angalizo mawakala feki elimu ya juu

Unguja. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kumekuwapo na wimbi la mawakala feki wanaowaliza wazazi na wanafunzi wakidai kuwapeleka kusoma vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi kumbe hawana sifa, hivyo kuwataka wajihadhari na utapeli huo. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (Wema), Abdugulam Hussein amesema hayo leo Julai 21, 2024 alipofunga…

Read More

MAOFISA USAFIRISHAJI (BODABODA ) WAJISAJILI KWENYE KANZI DATA KWA USALAMA -RPC LUTUMO

Mwamvua Mwinyi, Pwani Jeshi la Polisi Mkoani Pwani kwa kushirikiana na Maofisa usafirishaji Wilaya ya Kibaha (bodaboda), limezindua zoezi la uvaaji viakisi mwanga katika ili kuwa rasmi na kuepuka kukumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo kuporwa vyombo vyao vya moto. Akizungumza katika uzinduzi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ,Pius…

Read More

Kikwazo utekelezaji mikakati taasisi za umma chatajwa

Unguja. Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said amesema licha ya taasisi za Serikali kuandaa mikakati mizuri, inashindwa kutekelezwa kwa sababu mbalimbali ikiwamo watendaji wengi kutokuwa na uelewa wa mipango hiyo. Zena ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 22, 2024 wakati wa semina ya siku mbili ya makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, watendaji wakuu wa taasisi na…

Read More

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTENGUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:- B.i Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph…

Read More

ACT-Wazalendo yakemea siasa utekelezaji miradi

Unguja. Chama cha ACT-Wazalendo kimesema masuala ya kisiasa yanachangia kukwama miradi mikubwa ya maendeleo na kusababisha miradi ya mabilioni ya fedha za wananchi kukwama. Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Julai 21, 2024 kwenye Uwanja wa Mwenge, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja. Akiwahutubia wafuasi, wanachama na wananchi waliohudhuria mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa…

Read More

TPA yatekeleza maagizo ya Bodi ya TASAC Bandari ya Nyamisati

*Mkurugenzi Mkuu TASAC asema zaidi ya Bilioni Mbili kununua boti za Uokozi Na Chalila Kibuda ,Rufiji Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imesema maagizo walioyatoa kwa Mamlaka ya Bandari (TPA)katika Bandari ya Nyamisati yametekelezwa kwa asilimia 95. Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya ziara ya Bodi hiyo katika Bandari ya Nyamisati…

Read More

Kuna Maxi Nzengeli mmoja tu Yanga

BEKI wa kushoto wa FC Augsburg, Mads Pedersen ambaye msimu uliopita wa mashindano Ujerumani alicheza michezo 27 ya Ligi Kuu (Bundesliga) na moja ya Kombe la DFB-Pokal, ameukubali mziki wa winga Mkongomani wa Yanga, Maxi Nzengeli katika mchezo wa kirafiki ambao timu hizo zilikutana katika michuano ya Mpumalanga Premiers huko Afrika Kusini, mwishoni mwa wiki….

Read More

Masauni aonya wanafunzi matumizi ya dawa za kulevya

Unguja. Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amewaonya wanafunzi waliopo shuleni, vyuoni na taasisi nyingine za elimu kuacha kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya, ambazo husababisha nguvu kazi ya Taifa kupotea. Pia, ameitaka jamii kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika vita dhidi ya dawa za kulevya zinazoathiri maendeleo ya uchumi wa nchi….

Read More