
Simba yatoa msimamo ishu ya Kibu Denis
Uongozi wa Simba umepanga kumchukulia hatua za kinidhamu kiungo wake mshambuliaji, Kibu Denis kutokana na kushindwa kuwasili kwenye kambi ya timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine itakayoshiriki msimu ujao na badala yake amekuwa akitoa sababu tofauti kila siku. Simba kwa sasa iko jijini Ismailia, Misri…