Bunge la Bangladesh limevunjwa kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais, kufuatia masharti yaliyowekwa na waratibu wa maandamano ya wanafunzi. Wanafunzi hao walikuwa na makataa ya saa tisa (09:00 GMT) kwa serikali inayooongozwa na jeshi kujibu madai yao.
Wanafunzi wamesema hawatakubali serikali inayooongozwa na jeshi na wamepata idhini ya Muhammad Yunus, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, kuwa mshauri mkuu wa serikali ya mpito. Hali hiyo imeongeza mvutano, huku Chama cha Huduma ya Polisi ya Bangladesh (BPSA) kikitangaza mgomo hadi usalama wa maafisa wake utakapokuwa na uhakika.
BPSA, inayowakilisha maelfu ya maafisa wa polisi, imesema kuwa zaidi ya vituo 450 vya polisi vilishambuliwa siku ya Jumatatu na baadhi ya maafisa wa polisi waliuawa wakati wa maandamano yaliyokuwa yakishinikiza Waziri Mkuu Sheikh Hasina kujiuzulu. Mapema Jumanne, idhaa ya BBC Bangla iliripoti kuwa hakuna polisi wa trafiki kwenye barabara nyingi za mji mkuu Dhaka, huku wanafunzi wakielekeza trafiki katika baadhi ya maeneo.
#KonceptTvUpdates