Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la ufungaji wa mita za malipo ya kabla (prepaid meters) kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan alitoa kwa Wizara ya Maji kuanza matumizi ya teknolojia ya mita za malipo ya kabla kwa wateja ili kuboresha huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 7,2024 Kaimu afisa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire alisema kuwa lengo la kufunga mita za malipo ya maji kabla inalenga kuboresha huduma, kusaidia kupunguza changamoto za kihuduma za mara kwa mara kutoka kwa wateja na kupunguza changamoto za ankara kwa wananchi na hivyo kuleta ufanisi wa huduma zitolewazo na Mamlaka
Kwanamna nyingine Mhandisi Bwire ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwa kuwezesha kukamilishwa kwa mradi mkubwa wa kusambaza maji wa Chalinze awamu ya 3 uliogharimu Billioni 94 uliosaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutokalita Milioni 7.2 hadi lita 12.6 kwa siku.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire pia amezungumza na wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu hali ya upatikanaji wa majisafi na usafi wa Mazingira sambamba na kueleza mipango iliyopo ya kuboresha huduma ya maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na maeneo ya pembezoni
“Tumeona uwepo wa maji umeongezeka katika vyanzo vyetu vya maji na kazi kubwa inayofanywa na DAWASA bado ni kuboresha miundombinu ya uzalishaji maji ili huduma ifike kwa wananchi ipasavyo,”
‘tutaanza kuwawekea mita hizi mpya walio wadeni na watatakiwa kulipia madeni yao iliwafurahie huduma kama kawaida’